Mbunge wa Arusha mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema amekosa dhamana baada ya mawakili wa upande wa Jamhuri kuweka pingamizi kukata rufaa.
Mawakili wa Godbless walikusudia leo Dessemba 28, kuwasilisha hoja sita mahakamani kwa kusudio la kutaka mteja wao apewe dhamana, lakini hali imekuwa tofauti baada ya Jamhuri kupinga rufaa hiyo.
Lema alikamatwa Novemba 2 mjini Dodoma, tangu wakati huo, ameshikiliwa katika gereza kuu la Kisongo jijini Arusha ambako amekaa kwa siku 56 sasa.
Baada ya kukamatwa mbunge huyo alifikishwa mahakama ya hakimu mkazi Arusha, bwana Lema alipata dhamana na hakimu mkazi Desdery Kamugisha katika kesi namba 440 na 441/2016 akidaiwa kutoa lugha za uchochezi dhidi ya raisi wa awamu ya tano John Pombe Magufuli.