Baada
ya uchaguzi nchini Gambia, raisi mteule wa nchi hiyo Bwana Adam Barrow amesema
kuwa ni wakati wa kujenga Ghana yenye matumaini mpya.
Adama Barrow mwenye umri wa miaka 51, na ambaye ni tajiri
anayejishughulisha na biashara ya kujenga na kuuza majengo(nyumba), ameweza
kushinda baada ya matokeo kutangazwa siku ya ijumaa na mkuu wa tume ya uchaguzi
nchini Gambia, , Alieu Momarr Njai.
Barrow amemzidi Yahya kwa kura 51,416, ambapo kura za Barrow
zilikuwa ni 263,515(45.5%) na Yahya kupata kura 212,099(36.7).
Raisi anayeachia madaraka nchini humo bwana Yaya Jammeh amekiri kushindwa,
hii ni baada ya kumpigia Barrow na kumwahidi kumsaidia kujenga Gambia.
Yaya Jammeh ameweza kuingoza Gambia kwa miaka takribani 22, ambapo
aliichukua nchi kwa mabavu na kujisimikia uongozi wa juu wa nchi ya
Gambia(raisi).
Uchaguzi wa Gambia umewaacha wengi midomo wazi baada ya ushindi wa bwana Barrow kwa kile
ambacho hakikutarajiwa, kwani Adam Barrow ni mgeni katika siasa na kwa upande
wa Jammeh naye amekiri kushindwa jambo ambalo ni nadra kwa kiongozi mwenye
tabia za kidikteta(mabavu).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni