Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Tehama. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Tehama. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 24 Novemba 2016

Google, Facebook, Microsoft, Apple wavutiwa zaidi na roboti

Makampuni makubwa yanayotengeneza na kumiliki programu tofauti za kompyuta na simu, hivi karibuni yametangaza kuwa wamejikita katika ubunifu na uandaaji wa program roboti ambazo zitakazoweza kutumika katika kufanikisha kazi mbalimbali.


Kwa ujumla utengezaji wa roboti haujanza leo, ulianza mbali kuanzia miaka ya 1950 na 60. Na kwa wakati ule viliandaliwa pasipo ujengwaji mzuri wa grafiksi, japo ziliweza kuunganishwa katika mifumo ya kuratibu na kutoa huduma za mawasiliano ya papo(instant messaging services).


Kwa sasa zimeweza kuboreshwa pamoja na kuwa uweza wa kujibu maswali mbalimbali kwa watumiaji wake hasa kwa njia ya intaneti na kutoa majibu juu ya hayo maswali kwa njia iliyo sahihi.

Kwa nini Google, Facebook na Microsoft wavutiwe zaidi na utengezaji wa program roboti hizi..?

Haya makampuni yanaweza kufanya haya yote yakiwa na malengo mengi, haya ni baadhi tu:

⟾  Kwa kufuata mahitaji ya watumiaji wake(wateja).
⟾  Kwa kutaka kufanya mawasilano yawe mepesi na nafuu kwa watumiaji.
⟾  Kuweza kutumika kama watoa huduma wa mwanzo kwa wateja kabla       mwanadamu hajahusishwa, na mwadamu atahusishwa endapo ufumbuzi         wa tatizo halijapatikana kwa msaada wa programu roboti.
⟾  Programu hizi zinaweza kutumika zenyewe pasipo uendeshaji wa mtu, na                      kufanya huduma kuwa ya haraka na hakika hasa za kimwamala(benki) 

Apple ikiwa kama kampuni inayotengeneza vifaa vya teknolojia vitumiavyo umeme, kama vile simu, saa, kompyuta n.k wao wameweza kutengeneza programu roboti(Siri) ambayo hupatikana kwenye simu zao. Programu Siri, unaweza kumuuliza vitu ama ukamwomba aendeshe programu na akatoa majibu kulingana na maulizo yako, au akatoa mbadala wa kile unachokihitaji endapo kitakuwa hakipo.

Google nao wameweza kutengeneza programu roboti za namna tofauti, ikiwemo 
Google's web crawling bot (ama hufaamika kama "spider") ambayo huweza kukusanya taarifa kwa njia ya mtandao. Pia wamethubutu katika kutengeneza gari yenye uwezo wa kujiendesha yenyewe maarufu kama (Google Seft-Driving car).

Microsoft nao kwa sasa wanazo projekti nyingi wanazo shughulika nazo, lakini projekti yao maarufu ni ile programu roboti ijulikanayo kwa jina la 
Cortana, hii programu inapatikana kwenye programu yao kuu(os) kama vile Windows 10, Windows 10 Mobile, Windows Phone 8.1(windo toleo la kumi kwa kompyuta na simu na il ya toleo la 8.1)

Cortona inaweza kutoa majibu juu ya maswali yako kwa njia kuandika katika eneo la kuulizia (search engine) iwapo utakuwa umeunganisha kifaa(simu, komputa ama tableti-kibao) chako kwenye mtandao.

Facebook nao hawako nyuma, pia wamejikita zaidi katika kufanya tafiti maarufu kama 
Facebook AI Research (FAIR). Facebook wametengeneza vifaa maarufu kama vitual reality(ukweli uliotengenezwa) ambapo hii teknlojia imekusudiwa na facebook kutumika kwenye michezo ya gemu, kufanya mawasiliano ya kibishara, pamoja na kuona vitu ulivyonavyo mbali na kuhisi kama upo katika mazingira hayo. 

Mawasiliano yanayohusisha ujumbe wa papo(instant messaging) unaofanywa na makampuni kama WhatApp, Telegram, Hangouts, WeChat na Facebook messanger imepanuka kwa sasa na kuunganisha dunia kama kijiji.

Ijumaa, 4 Novemba 2016

Huawei imekaribisha kifaa kipya, jina lake Mate 9

Huawei imezindua simu mpya yenye skrini kubwa kiasi cha inchi 5.9.
Simu hiyo lijulikanlo kwa jina la Mate 9, ni kati ya simu za kwanza zinazotumia teknolojia ya Androidi 7.
Na imekuja ikiwa katika aina mbili za kamera za nyuma simu.
Ambapo kamera moja ikiwa na migapikseli 20MP, na myingine ni migapikseli 12MP.
Vile vile simu hi ya Huawei Mate 9, imekuja na kamera ya mbele yenye uwezo wa migapikseli 8MP. 
Pia simu hii inasapoti generesheni zote za muunganiko wa mtandao kama vile 2G, 3G, 4G n.k.

Sifa kuu ya simu ya smatfoni brandi ya Huawei Mate 9.

- 5.9 inch screen, 1920 x 1080 pixel display
- HUAWEI Hisilicon 960 octa core
- 4GB RAM, 64GB ROM
- 20MP+12MP rear camera, 8.0MP front camera
- OS, Android V 7.0 (Nougat)
- CPU Octa-core (4x2.4 GHz Cortex-A73 & 4x1.8 GHz Cortex-A53)
- GPU Mali-G71 MP8
- Battery Non-removable Li-Po 4000 mAh battery

Huawe Mate 9 katika muonekano tofauti