Jumatano, 28 Desemba 2016

Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya 9 kwa 2016

Mwanasoka wa wa kimataifa, Cristiano Ronaldo wa nchi ya Ureno, ambaye anachezea klabu ya mpira ya Raal Madrid ya Hispania anakamilsha mwaka wa 2016 kwa kushinda tuzo yake ya tisa.
Bwana Cristiano alifanikiwa  kushinda tuzo hiyo iliyojulikana kama Globe Soccer Award hapo Dubai.

Tuzo hii ya mkata kabumbu bora wa dunia (Globe Soccer Award) kwa mwaka huu wa 2016 imekuwa ni tuzo ya 9 kwa Cristiano kwa mwaka huu wa 2016, hii ni baada ya kujishindia tuzo kadha wa kadha, ikiwamo, The World Soccer Award, Four Four Two, Espy, Di Stéfano Award, Goal.com, FIFA Club Golden Ball, na Ballon d'Or.

Katika tuzo hiyo ya Globe Soccer Award 2016 aliyoibuka Ronaldo mshindi ilikuwa pia ikiwania na wachezaji kama Lionel Messi, Gonzalo Higuan, Antonie Griezmann, Jamie Vardy, mwanasoka huyu ameweza kushinda tuzo hizo kwa mara ya nne sasa, hii ni miaka tofauti ambayo amewvza pia kushinda tuzo hizi 2011, 2013 na 2014.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni