Jumamosi, 3 Desemba 2016

Baada ya Uchaguzi nchini Gambia, Barrow asema..

Baada ya uchaguzi nchini Gambia, raisi mteule wa nchi hiyo Bwana Adam Barrow amesema kuwa ni wakati wa kujenga Ghana yenye matumaini mpya.
Adama Barrow mwenye umri wa  miaka 51, na ambaye ni tajiri anayejishughulisha na biashara ya kujenga na kuuza majengo(nyumba), ameweza kushinda baada ya matokeo kutangazwa siku ya ijumaa na mkuu wa tume ya uchaguzi nchini Gambia, , Alieu Momarr Njai.

Barrow amemzidi Yahya kwa kura 51,416, ambapo kura za Barrow zilikuwa ni 263,515(45.5%) na Yahya kupata kura 212,099(36.7).

Raisi anayeachia madaraka nchini humo bwana Yaya Jammeh amekiri kushindwa, hii ni baada ya kumpigia Barrow na kumwahidi kumsaidia kujenga Gambia.


Yaya Jammeh ameweza kuingoza Gambia kwa miaka takribani 22, ambapo aliichukua nchi kwa mabavu na kujisimikia uongozi wa juu wa nchi ya Gambia(raisi).

Uchaguzi wa Gambia umewaacha wengi midomo wazi baada ya ushindi wa bwana Barrow kwa kile ambacho hakikutarajiwa, kwani Adam Barrow ni mgeni katika siasa na kwa upande wa Jammeh naye amekiri kushindwa jambo ambalo ni nadra kwa kiongozi mwenye tabia za kidikteta(mabavu).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni