Jumatano, 28 Desemba 2016

Hoja sita za Mbunge Godbles Lema kusikilizwa leo

Hoja sita za mawakili wa mbunge wa Arusha mjini (Chadema), Godbles Mlema kupinga kunyimwa dhamana zinatarajiwa kusikilizwa leo mbele ya mahakama kuu jijini Arusha.
Wakili Sheck Mfinanga anayemwakilisha Lema alisema waliwasilisha hoja hizo za rufaa kupinga uamuzi wa kunyimwa dhamana mteja wao.

Mbunge Lema anashikiliwa katika gereza kuu la Kisongo jijini Arusha tangu akamatwe Novemba 2 mwaka huu mjini Dodoma. Na sasa amekaa siku kwa 56.

Mara baada ya ya kukamatwa na kufikishwa mahakama ya hakimu mkazi Arusha, Lema alipewa dhamana na hakimu mkazi Desdery Kamughisha katika kesi namba 140 na141/ 2016 akidaiwa kutoa kauli za uchochezi dhidi ya raisi John Pombe Magufuli.

Hata hivyo, mkurugenzi wa mashitaka DPP alikata rufaa ya kupinga uamuzi wa mahakama kumpa dhamana Godbles Lema.

Hali imepelekea mawakili wa Lema nao kukata rufaa ya kupinga mteja wao kunyimwa dhamna, ili kesi isikilizwe tena leo baada ya kukwama kwa mda mrefu kutokana na kuwapo pingamizi nyingi za kisheria zilizowasilishwa na upande wa pili wa kesi (Jamhuri).










Hakuna maoni:

Chapisha Maoni