Makampuni
makubwa yanayotengeneza na kumiliki programu tofauti za kompyuta na simu, hivi
karibuni yametangaza kuwa wamejikita katika ubunifu na uandaaji wa program roboti
ambazo zitakazoweza kutumika katika kufanikisha kazi mbalimbali.
Kwa ujumla utengezaji wa roboti haujanza leo, ulianza mbali kuanzia miaka ya 1950 na 60. Na kwa wakati ule viliandaliwa
pasipo ujengwaji mzuri wa grafiksi, japo ziliweza kuunganishwa katika mifumo ya
kuratibu na kutoa huduma za mawasiliano ya papo(instant messaging services).
Kwa sasa
zimeweza kuboreshwa pamoja na kuwa uweza wa kujibu maswali mbalimbali kwa
watumiaji wake hasa kwa njia ya intaneti na kutoa majibu juu ya hayo maswali
kwa njia iliyo sahihi.
Kwa nini Google, Facebook na Microsoft wavutiwe zaidi na
utengezaji wa program roboti hizi..?
Haya makampuni yanaweza kufanya haya yote yakiwa na malengo mengi, haya ni
baadhi tu:
⟾
Kwa kufuata mahitaji ya watumiaji wake(wateja).
⟾
Kwa kutaka kufanya mawasilano yawe mepesi na nafuu kwa watumiaji.
⟾ Kuweza
kutumika kama watoa huduma wa mwanzo kwa wateja kabla mwanadamu hajahusishwa, na mwadamu
atahusishwa endapo ufumbuzi wa tatizo halijapatikana kwa msaada wa programu roboti.
⟾ Programu hizi zinaweza kutumika zenyewe pasipo
uendeshaji wa mtu, na kufanya huduma kuwa ya haraka na hakika hasa za kimwamala(benki)
Apple ikiwa kama kampuni inayotengeneza vifaa vya teknolojia
vitumiavyo umeme, kama vile simu, saa, kompyuta n.k wao wameweza
kutengeneza programu roboti(Siri) ambayo hupatikana kwenye simu
zao. Programu Siri, unaweza kumuuliza vitu ama ukamwomba aendeshe programu na
akatoa majibu kulingana na maulizo yako, au akatoa mbadala wa kile
unachokihitaji endapo kitakuwa hakipo.
Google nao wameweza
kutengeneza programu roboti za namna tofauti, ikiwemo Google's web crawling bot (ama
hufaamika kama "spider") ambayo huweza
kukusanya taarifa kwa njia ya mtandao. Pia wamethubutu
katika kutengeneza gari yenye uwezo wa kujiendesha yenyewe maarufu kama (Google
Seft-Driving car).
Microsoft nao kwa
sasa wanazo projekti nyingi wanazo shughulika nazo, lakini projekti yao maarufu
ni ile programu roboti ijulikanayo kwa jina la Cortana, hii
programu inapatikana kwenye programu yao kuu(os) kama vile Windows 10, Windows 10 Mobile, Windows Phone 8.1(windo toleo la
kumi kwa kompyuta na simu na il ya toleo la 8.1)
Cortona inaweza kutoa
majibu juu ya maswali yako kwa njia kuandika katika eneo la kuulizia (search engine) iwapo
utakuwa umeunganisha kifaa(simu, komputa ama tableti-kibao) chako kwenye
mtandao.
Facebook nao hawako nyuma, pia wamejikita zaidi katika
kufanya tafiti maarufu kama Facebook AI
Research (FAIR). Facebook wametengeneza vifaa maarufu kama vitual reality(ukweli
uliotengenezwa) ambapo hii teknlojia imekusudiwa na facebook kutumika kwenye michezo
ya gemu, kufanya mawasiliano ya kibishara, pamoja na kuona vitu ulivyonavyo
mbali na kuhisi kama upo katika mazingira hayo.
Mawasiliano yanayohusisha ujumbe wa papo(instant messaging)
unaofanywa na makampuni kama WhatApp, Telegram, Hangouts, WeChat na Facebook messanger imepanuka
kwa sasa na kuunganisha dunia kama kijiji.