Ndoa ni
kiungo pekee katika maisha ya mwandamu, na maisha
yanaweza kuwa ya ajabu sana katika uso wa dunia endapo hakutakuwa na
muunganiko wowote wa watu wawili wenye jinsia tofauti mbili (mwanamme na mwamke)
na hawa kuridhia katika kuoana na kuishi pamoja kama mume na mke.
Duniani kumekuwa na ndoa nyingi, zikiwemo za gharama za chini,
katikati na juu.
Hebu leo tutazame ndoa za mastaa duniani ambazo zimeweza kuweka rekodi duniani kwa kuwa ghali zaidi.
Mpangilo huu upo katika orodha ya ishirini kushuka mpaka ya kwanza(top 20).
#20 Nicole Kidman & Keith Urban
Ndoa hii ilifungwa katika kanisa la katoliki (cliff-top Roman Catholic Church) uliopo katika mji wa Sydney, kwao Kidman nchini Australia, juni 25, 2006.
Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - $250,000
#19 Marc Anthony & Dayanara Torres
Baada ya kufunga ndoa ya ghafla huko Vegas, Mei 2000, Hawa wawili waliweza kufunga ndoa rasmi na kubwa katika viunga vya San Juan uiopo katika mji wa Puerto Rico hapo baadae disemba 2002.
Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - $500,000
#18 Tommy Mottola & Mariah Carey
Ndoa hii ilifungwa kati ya mwanamuziki Maria Carey na aliyekuwa mfanyakazi katika kampuni ya Sony Music, bwana Tommy Mottola mwezi juni 1993. Ndoa kufungwa katika kanisa la St. Thomas Episcopal. Ndoa hii inatafisiriwa kuwa na hadhi ya kifalme.
Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - $500,000
#17 Dario Franchiti & Ashley Judd
Hawa wawili waioana mnamo mwaka wa 2001 katika kasiri ya Skibo uliopo Skotilndi, Judd na Franchiti walihitaji kitu, mahusiano ya karibu. Cha ajabu hawa wendanao waliweza kukodi vyumba 40 katika kasiri na kugharimu dola la marekani $35,000/ kwa siku nne walizokaa hapo.
Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa :- $750,000
#16 David Beckham & Victoria Adams
Walioana Julai 1999 katika kasiri ya Luttrellstown karibu na Dublin, hii ndoa ni mwana kandanda maarufu and aliyekuwa mwanamziki wa kundi la Spice Girl na tarajio lao lilikuwa wafunge ndoa yenye hadhi ya kimalkia na kifalme. Na ndicho walichokifanya kwani sherehe yao ya ndoa ilifana sana na kuwa kama walipnda iwe.
Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - $800,000
#15 Brad Pitt & Jennifer Aniston
Ilikuwa ni ndoa ya aina yake kwa mwaka wa 2000, July 29 kati ya hawa mastaa na waigizaji wa hollywood iliyofanyika katika viwanja vya Malibu ya mwandaaji wa televisheni, Marcy Carsey. Na kila aliyehusika na kuhudhuria alitakiwa kusaini dola milioni $1 kwa ajili ya kuhifadhi unyeti wa swala. pia sherehe ilipndezeshwa busatni nzuri yenye maua mazuri bi ghali, na inasmkana idadi ya maua ilikuwa kama 50,000 na kumulikwa na mishumaa meupe yakimulika ema zuri lililokuwa katika eneo la mapokezi.
Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milioni $1
# 14 Tori Spelling & Charlie Shanian
Hii pia ni sherehe ya ndoa kati ya hawa wapendanao, Tori Spelling & Charlie Shanian iliyofanyika julai 2004. Maharusi hawa walipendeza kwa mavazi yao ya bei ghali na shela nzuri yenye bei ghali, huku mapambo mazuri ya glasi, mbao na mawe yakiwa yametawala mazingira na nakshi nzuri za maua zenye madini ya almasi zilizovaliwa kuficha uso wa maharusi.
Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milioni $1
# 13 Donald Trump & Melania Knauss
Mfanyabiashara wa mali zisizohamishika mogul na mwanamitindo walifunga pingu za maisha katika kanisa la Episcopal lilipo katika kingo za bahari huko Bethesda mnamo mwezi wa januari 2005. Mavazi ya maharusi ndiyo aliyokuwa jambo la kuongelea hapo, na kuteka mjadala. Na mavazi ya bibi harusi yaliandalia kwa namna nzuri na kugharimu pesa nyingi sana. Na baada ya sherehe, magari maarufu kwa jina la limo, wageni walisafirishwa kutoka kanisani mpaka ukumbi wa hadhi uliopo katika viunga vya Mar-a-Lago estate unaomilikwa na bwana harusi Trump, wenye thamani dola milioni $42. Huku katika sherehe hizo zikitawaliwa na wanamuziki na watumbuizaji bendi kubwa duniani.
Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : milioni $1
#12 Madonna & Guy Ritchie
Hii ndoa ilikuwa imerembwa na maarufu kati ya wawili hawa. Walipata kuoana desemba 2000 huko Skotilandi katika kasiri ya skibo. Ndoa ilijikita katika mahusiano yasiyo ya siri, ambapo hawa wapendwa waliweza kukodi kasiri nzima, ikiwemo kukodi vyumba vyote vya wageni, pamoja na walinzi wapatao 70 na wahudumu. Bibi harusi akiwa amevalia mavazi ya ghali zaidi kwa yakiwa na nakshi ya almasi ambapo inasvmekana iliwahi kuvaliwa na malkia Grace wa Monaco. Huko bwana harusi Guy Ritchie amevalia vazi zuri ya kilti.
Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milioni $1.5
#11 Pierce Brosnan & Keely Shaye Smith
Muigizaji na mwandishi wa habari wa runinga nje ya miinuko ya Irelandi ogasti 2001. Huko mapokezi yakipambwa na desturi za watu wa Ireland(Irish), vyakula na michzo ikwa ya tamaduni ya watu wa jamii hiyo katika kasiri ya Ashford liloko pwani. Huko bibi na bwana arusi wakiwa katika mavazi yao ya nguvu na ghali zaidi.
Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milioni $1.5
#10 Eddie Murphy & Nicole Mitchell
Mcheshi na bibi harusi waliweza kuoana Hotli ya New York Plaza mnamo 1993. Zaidi ya wageni 500 waliohudhiria ukumbini hapo, ukumbi ulipambwa zulia jeupe na maua mazuri yakitanda eneo la tukio. Baada ya sherehe ya harusi pale ukumbini, wageni waalikwa waliweza kupata chakula na vinywaji vya gharam za juu.
Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milioni $1.5
#9 Tiger Woods & Elin Nordegren
Mchezaji wa golf mwanamitindo wa Swedeni walioana mwaka 2004 katika bichi ya Sandy Lane Beach Resort huko Barbados. Ili kuona ndoa yao inafanikiwa kama walivyotaka hawa wawili waliwza kukodi hii shmu ya starehee na vyumba vaak vyote200 ambayo iligharimu dola $1 laki mbili. Huku mapokezi ikipambwa na mziki mzuri na mapambo ya thamani sana.
Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milioni $1.5
#8 Michael Douglas & Catherine Zeta-Jones
Ilikuwa nayo ni moja ya ndoa zilizotia fora, kwa maana vyombo vya habari vilimzunguka bwana harusi Douglas na bi haarusi Zeta-Jones mpaka sherehe ya harusi ilipofika ukingoni. Maharusi walichagua kufunga pingu za maisha katika hoteli maarufu kwa jina la Plaza Hotel huko New Yorks Novemba, 2005. Ili wanandoa waweze kuvinjari pasipo shida wakamua kukodi walinzi 50 wakiwemo askari polisi 30. Huku wageni waalikwa wakiwa wanawasili ukumbini kwa kadi zilizoandalia kwa nakshi nzuri za madini.
Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milioni $1.5
#7 Elton John & David Furnish
Mwanamziki nguli wa mziki jamii ya pop na muaandaji filamu walipata kufunga ndoa desemba 200 wiki hiyo ya kwanza ambapo ndoa za jamii wanaounga ndoa za jinsia moja ilipopitishwa kisheria huko nchini Uingereza. Hawa wawili waliweza kubadilishana mawili matatu katika ukumbi mmoja mkubwa na mashuhuru hapo nchini Uingereza ujulikanao kwa jina la Windsor's Guildhall, ambapo mtoto wa kiume wa kifalme Prince Charles na Camilla Parker Bowles walipata kuoana miezi 8 iliyopita. Zaidi ya wageni 600 waliohalikwa walihudhuria wakala na kunywa chakula na vinywaji vya gharama, ambapo inakadiria kila kinywaji maarufu kama vintage pink champagne iligharimu dola $ 300 kwa kila chupa.
Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milioni $1.5
#6 Christina Aguilera & Jordan Bratman
Baada ya Bratman kumwomba uchumba siku ya wapendanao (Valentine's Day) huko Carmel. Wawili hawa waliweza kubadilishana maneno mawili matatu katika bonde moja maarufu kama "Napa Valley's Staglin Family Vineyard" mnamo Novemba 2005. Wawili hawa walipata kupumzika katika vibanda vya Auberge du Soleil, vinavyodaiwa kugharimu dola $3,500 kwa usiku mmoja, vikiwa na moto uliokokwa nje yao. Lakini ndoa halisi ilifanyika katika mahema yaliopo katika sehemu iliyozungukwa na barafu. Na maua ya aina mbalimbali kama rose, shaba, almasi n.k yakitawala mandhari hayo pia.
Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milioni $2
#5 Elizabeth Taylor & Larry Fortensky
Elizabeth Taylor aliweza kuoana mume wake wa saba ikiwa ni moja ya ndoa iliyofujisha hela nyingi sana. Wawili hawa walikutana huko kliniki ya Betty Ford Clinic, na kuoana Octoba 6, 1991 katika ranchi moja ya Michael Jackson's Neverland Ranch. Pia wawili hawa waliweza kuuza baadhi ya picha zao za sherehe maarufu kwa bei ghali zaidi ya dola milioni $1 kwa kampuni moja ya habari maarufu kwa jina la "People Magazine" ambapo hela hiyo waliigeuza kuwa mchango kwa waathirika wa Ukimwi (AIDS charities).
Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milioni $2
#4 Tom Cruise & Katie Holmes
Ndoa ya TomKat ilivuma na kuwa kama ndoa ya mwaka 2006. Wawili walipata kuoana Novemba nchini Itali katika kasiri ya 15th-century Odescalchi Castle uiopo nje mwa mji wa Rome. Waandishi wa habari walilijaza eneo la tukio. Wote bwana na bibi harusi wakivalia mavazi yaliosanifiwa na msanifu mavazi Giorgio Armanai kwa thamani nyingi sana. Wageni waalikwa wakiwa wakijivinjari na chocolate nyeupe, keki ya harusi na 300 chupa ya vinywaji za wine. Burudani za musiki wa okstra (orchestra ).
Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milioni $2
#3 Elizabeth Hurley & Arun Nayar
Mwanamitindo na muigizaji wa filamu pamoja na mfanyabiashara wa kihindi walipata kuoana Machi 2007 huko sherehe ikiwa ikiendelea kwa siku 8 na kuvuka mabara mawili. Sherehe ya kwanza ilifanyika Machi 2 katika kasiri ya Sudeley Castle huko mjini Gloucestershire. Baada ya sherehe yao huko Uingereza waliweza kuamia nchini India mnamo Machi 9, ambapo sherehe za harusi zikafanyika katika tamaduni na desturi za kiindi na hii sherehe hii ilifanyika Umaid Bhawan Palace katika jiji la Jodhpur, India. Ambapo hawa wawili waliweza kupumzika katika hilo jumba la kifaari kwa dola $10,000 kwa usiku mmoja.
Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milioni $2.5
#2 Paul McCartney & Heather Mills
Aliyekuwa muimbaji wa mziki wa rock katika bendi ya Beatles(Beatles band) aliomba uchumba kwa mwanamitindo Heather Mills mnamo 2001 kwa kumvisha pete ya uchumba ya almasi. Na baadae kuoana mwezi Juni 2002 kanisani St. Salvador's Church huko Monaghan, nchini Ireland. Maarusi walimachi baina ya viti hapo kanisani huku ukiimbwa wimbo wa McCartney aliomwandikia mchumba wake wenye jina la "Heather". Mapokezi yaliandaliwa na kupambwa kwa hadhi ya kihindi iliyofanyika huko kingo ya ziwa, huku watumbuizaji wa muziki wakivalia kwa tamaduni za kihindi, na kupata milo ya watu wa jamii ya kivejitariani(vegetarian feast).
Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milioni $3
#1 Liza Minelli and David Gest
Mshindi wa tuzo za Oscar na mwigizaji, mwandaaji wa vipindi wa runinga walioana Machi 2002 kanisani Manhattan's Collegiate Church. Tukio la ndoa yao ilivuma sana, ambapo Best Man alikuwa ni Michael Jackson (ambaye ni rafiki wa karibu wa Minelli) na matroni wa bibi harusi alikuwa Elizabeth Taylor. Jackson aliambatana na Minelli wakitembea baina ya viti mle kanisani, huku wimbo wa muimbaji na mtunzi wa nyimbo Natalie Cole alipoimba wimbo wake maarufu kwa jina la "Unforgettable". Wageni waalikwa wa Minelli na Gest walikadiriwa walikadiriwa kiasi 850 ambapo waliweza kuhudumiwa vizuri. Keki ya ndoa ya ngazi 12 ikipambwa na picha ya bwana na bibi harusi. Wakati huo mziki mkubwa wa okestra(orchestra), na wasanii na waimbaji wengi kama Tony Bennett, Stevie Wonder na Natalie Cole wakitoa burudani ya kukata na shoka. Baadhi ya wafanyakazi wapatao 500 waliajiriwa kwa kuhakikisha sherehe inastawi na ulinzi umehimarika eneo la tukio. Na hii ndiyo ndoa inayokadiriwa kuwa ghali zaidi kuliko za hawa watu maaarufu(mastaa) duniani. Hata hivyo hii ndoa ya hawa wawili haikupata nafasi ya kuishi kwa mda mrefu, kwani ilivunjika mwaka uliofuatia.
Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milion $3.5
Chanzo cha habari ni romancefromtheheart.com na Forbes.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni