Vyuo feki sasa kufutwa na Serikali.
Serikali
ya Jamhuri ya Mhungano wa Tanzania imeweza kubaini uwepo wa vyuo vikuu lukuki
ambavyo havina sifa.
Hivyo
inakusudia kuvifuta hii ni kwa kutaka kuimarisha kiwango cha elimu inayotolewa
na ngazi zote nchini.
Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia, Profesa Joyse
Ndalichako ameyasma hayo jana siku ya jumatatu, Novemba 21, 2016, alipokuwa
akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau wa elimu ya juu, jijini Dar-es-salaam.
Mheshimiwa
waziri amesema hayo yamebainika baada ya jopo la wataalamu kufanya uhakiki humo
vyuoni.
Profesa
akasema, "Lengo ni kuhakikisha wasomi wanaohitimu kwenye vyuo hivyo,
wanakuwa wameiva kitaaluma, ili pia waweza pia kushiriki katika kuijenga
Tanzania ya viwanda".
Pia,
Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya vyuo vikuu nchini(TCU) Profesa Jackobo
Mtabaji, Amesema wamejipanga kuhakikisha kuwa wanafanya kazi zao kwa kusimamia
mwongozo uliopo ili kuondoa mara moja huu uwepo wa vyuo vingi ambavyo havina
sifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni