Ijumaa, 4 Novemba 2016

Novemba 8, 2016 kuamua nchini Marekani

Novemba 8, 2016 ni siku ambayo wana taifa la Marekani watapiga kura ili kuamua ni nani kati bwana Donald Trump ama bi Hillary Clinton aweze kupokea kijiti toka kwa mhe. Barack Obama ambaye bado ndiye raisi wa taifa hilo.



Dunia nzima, macho na masikio yote yataelekezwa huko nchini Marekani ili kufuatilia nani ameweza kusafiri salama na kuingia katika malango ya ikulu ya taifa kubwa la Marekani.

Mpaka sasa, kuna ushindani mkali ambao upo kati ya wagombea wawili ambao ni bi. Hillary Clinton anayepeperusha chama Democrats na bwana Donald Trump anayeperusha chama cha  Republican. Wagombea wote wamaonekana kuuza zera zao kwa wamarekani kwa udi na uvumba kwa masaa machache yalobaki ili kura ipigwe.

Hata hivyo kumeonesha majimbo kadhaa ambayo yana ushindani mkali kati ya hawa wagombea wawili.

Chini hapa ni majimbo yenye ushindani mkali ambapo yamebainishwa kwa asilimia za ushindani kwa wagombea hawa wawili nguli, Hillary na Trump  kupitia utafiti wa maoni.

Arizona - Clinton(44%), Trump(47%)
Colorado - Clinton(43%), Trump(41%) 
Florida - Clinton(45%), Trump(46%)
Georgia - Clinton(42%), Trump(48%)
Iowa - Clinton(40%), Trump(42%)
Michigan - Clinton(46%), Trump(40%)
Nevada - Clinton(44%), Trump(46%)
New Hampshire - Clinton(44%), Trump(41%)
Karolina Kaskazini- Clinton(46%), Trump(46%)
Ohio - Clinton(43%), Trump(46%)
Pennsylvania - Clinton(47%), Trump(43%)
Virginia - Clinton(47%), Trump(42%)
Wisconsin - Clinton(47%), Trump(41%)

Utafiti umetolewa na Real Clear Politics. Na Zijue izi imekuletea ili nawe ujuwe.

Chochote kinaweza kubadilisha matokeo haya ya utafiti wa kisayansi ulofanywa na real clear politics. Fuatilia kwa karibu uchaguzi hapa katika blog yako ya Zijue izi, tutakuwa tunakujulisha kwa kadri tutakapokuwa tunapata habari mpya.

Asante kwa kutembelea blog hii ya Zijue izi www.zijueizi.blogspot.com, karibu tena.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni