Alhamisi, 24 Novemba 2016

Google, Facebook, Microsoft, Apple wavutiwa zaidi na roboti

Makampuni makubwa yanayotengeneza na kumiliki programu tofauti za kompyuta na simu, hivi karibuni yametangaza kuwa wamejikita katika ubunifu na uandaaji wa program roboti ambazo zitakazoweza kutumika katika kufanikisha kazi mbalimbali.


Kwa ujumla utengezaji wa roboti haujanza leo, ulianza mbali kuanzia miaka ya 1950 na 60. Na kwa wakati ule viliandaliwa pasipo ujengwaji mzuri wa grafiksi, japo ziliweza kuunganishwa katika mifumo ya kuratibu na kutoa huduma za mawasiliano ya papo(instant messaging services).


Kwa sasa zimeweza kuboreshwa pamoja na kuwa uweza wa kujibu maswali mbalimbali kwa watumiaji wake hasa kwa njia ya intaneti na kutoa majibu juu ya hayo maswali kwa njia iliyo sahihi.

Kwa nini Google, Facebook na Microsoft wavutiwe zaidi na utengezaji wa program roboti hizi..?

Haya makampuni yanaweza kufanya haya yote yakiwa na malengo mengi, haya ni baadhi tu:

 Kwa kufuata mahitaji ya watumiaji wake(wateja).
 Kwa kutaka kufanya mawasilano yawe mepesi na nafuu kwa watumiaji.
 Kuweza kutumika kama watoa huduma wa mwanzo kwa wateja kabla       mwanadamu hajahusishwa, na mwadamu atahusishwa endapo ufumbuzi         wa tatizo halijapatikana kwa msaada wa programu roboti.
  Programu hizi zinaweza kutumika zenyewe pasipo uendeshaji wa mtu, na                      kufanya huduma kuwa ya haraka na hakika hasa za kimwamala(benki) 

Apple ikiwa kama kampuni inayotengeneza vifaa vya teknolojia vitumiavyo umeme, kama vile simu, saa, kompyuta n.k wao wameweza kutengeneza programu roboti(Siri) ambayo hupatikana kwenye simu zao. Programu Siri, unaweza kumuuliza vitu ama ukamwomba aendeshe programu na akatoa majibu kulingana na maulizo yako, au akatoa mbadala wa kile unachokihitaji endapo kitakuwa hakipo.

Google nao wameweza kutengeneza programu roboti za namna tofauti, ikiwemo 
Google's web crawling bot (ama hufaamika kama "spider") ambayo huweza kukusanya taarifa kwa njia ya mtandao. Pia wamethubutu katika kutengeneza gari yenye uwezo wa kujiendesha yenyewe maarufu kama (Google Seft-Driving car).

Microsoft nao kwa sasa wanazo projekti nyingi wanazo shughulika nazo, lakini projekti yao maarufu ni ile programu roboti ijulikanayo kwa jina la 
Cortana, hii programu inapatikana kwenye programu yao kuu(os) kama vile Windows 10, Windows 10 Mobile, Windows Phone 8.1(windo toleo la kumi kwa kompyuta na simu na il ya toleo la 8.1)

Cortona inaweza kutoa majibu juu ya maswali yako kwa njia kuandika katika eneo la kuulizia (search engine) iwapo utakuwa umeunganisha kifaa(simu, komputa ama tableti-kibao) chako kwenye mtandao.

Facebook nao hawako nyuma, pia wamejikita zaidi katika kufanya tafiti maarufu kama 
Facebook AI Research (FAIR). Facebook wametengeneza vifaa maarufu kama vitual reality(ukweli uliotengenezwa) ambapo hii teknlojia imekusudiwa na facebook kutumika kwenye michezo ya gemu, kufanya mawasiliano ya kibishara, pamoja na kuona vitu ulivyonavyo mbali na kuhisi kama upo katika mazingira hayo. 

Mawasiliano yanayohusisha ujumbe wa papo(instant messaging) unaofanywa na makampuni kama WhatApp, Telegram, Hangouts, WeChat na Facebook messanger imepanuka kwa sasa na kuunganisha dunia kama kijiji.

Kumbe bi Hillary Clinton aliweza kushinda kwa kura nyingi.

Uchaguzi uliofanyika nchini Marekani wiki mbili zilizopita ambao ulishirikisha vyama kadha wa kadha, vikiwemo vyama viwili nguli, chama cha Republican kilichowakilishwa na bwana Donald Trump, na kile cha Democtrats ambapo wao walimsimisha bi Hillary Clinton kupeperusha bendera yake. 

Taarifa zimesema kuwa, kura za Clinton zimeongezeka mpaka milioni 2 kwa kura za kawahida. Japo katika huo uchaguzi wa Novemba 8, Trump alishinda kwa kuwa na kura nyingi za wajumbe,

Hivyo basi kwa sera na utaratibu wa nchi ya Marekani idadi kubwa ya kura za wajumbe ndizo huamua nani ni mshindi katika uchaguzi.

Hata hivyo baadhi ya watu wa kada mbalimbali wakiwemo wasomi, mawakili, na wanatakwimu wameweza kumshauri bi Clinton ili kuchungaza uhesabuji wa kura katika baadhi ya maeneo(majimbo) ambako kura ziliweza kupigwa na uhesabuji wake kufanyika kwa njia ya teknolojia ya komputa na ile ya kutumia njia ya desturi(makalatasi, kalamu, na skana).

Labda Clinton na timu yake itaweza kufanya hivyo kutokana na ushauri aliopata, japo kwa sasa hakuna lolote ambalo wameweza kulifanya.


MATOKEO YA URAISI kwa ujumla, kura zilizopigwa(%) na za wajumbE


Clinton 48.1% (232)Trump 46.6% (290)Johnson 3.3%Stein 1.0%
McMullin 0.4%









Democrats
Republican


Jumatano, 23 Novemba 2016

Samata na Wanyama nje Tuzo za CAF.

Shirikisho la soka barani Afrika CAF limeachia orodha ya wasaka kandanda watano ambao wataweza kushindania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2016.
Orodha hii imeamuliwa na kura za wajumbe wa kamati ya vyombo vya habari vinavyotambuliwa na CAF, na kamati ya maendeleo ya ufundi ya CAF, pamoja na jopo la wataalamu ambao huwa ni nusu ya 20(watu 10). Tuzo hizo zitafanyika January 5 2017, mjini Abuja Nigeria.
Wafuatao ni orodha ya wachezaji watakaoshindania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika wa Mwaka,
  •        Pierre-Emerick Aubameyang  (Gabon na Borrusia Dortmund)

  •       Riyad Mahrez (Algeria na Leices)

  •      ➤ Sadio Mane (Senegal na Liverpool)

  •       Mohamed Salah (Egypt na Roma)

  •       Islam Slimani (Algeria na Leicester).

Mbwana Ally Samatta, ni mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayechezea soka ya kulipwa Ubelgiji ni miongoni mwa wachezaji aliyekuwa kwenye orodha ya wachezaji 30 ambao walipata kuteuliwa kushindania tuzo ya shirikisho la soka barani Afrika (CAF) ya Mchezaji Bora wa Afrika katika awamu ya kwanza kabla ya wachezaji hao kupunguzwa hadi watano.
Victor Wanyama, ambaye ni kapteni wa timu ya taifa la Kenya, na kwa sasa anachezea klabu ya Tottenham. Mchezaji huyu naye alikuwa kwenye orodha iliyoteuliwa na CAF kabla ya mchujo huo haujatokea.
Wafuatao ni orodha ya wachezaji watakaoshindania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika wa Mwaka anayecheza ligi za ndani ya Afrika,
    Khama Billiat (Mamelodi Sundowns na Zimbabwe)
    Keegan Dolly (Mamelodi Sundowns na South Africa)
    Rainford Kalaba (TP Mazembe na Zambia)
    Hlompho Kekana (Mamelodi Sundowns na South Africa)
    Denis Onyango (Mamelodi Sundowns na Uganda).

Jumatatu, 21 Novemba 2016

Kiama Cha Vyuo Feki Nchini

Vyuo feki sasa kufutwa na Serikali.

Serikali ya Jamhuri ya Mhungano wa Tanzania imeweza kubaini uwepo wa vyuo vikuu lukuki ambavyo havina sifa.

Hivyo inakusudia kuvifuta hii ni kwa kutaka kuimarisha kiwango cha elimu inayotolewa na ngazi zote nchini.

Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia, Profesa Joyse Ndalichako ameyasma hayo jana siku ya jumatatu, Novemba 21, 2016, alipokuwa akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau wa elimu ya juu, jijini Dar-es-salaam.

Mheshimiwa waziri amesema hayo yamebainika baada ya jopo la wataalamu kufanya uhakiki humo vyuoni.

Profesa akasema, "Lengo ni kuhakikisha wasomi wanaohitimu kwenye vyuo hivyo, wanakuwa wameiva kitaaluma, ili pia waweza pia kushiriki katika kuijenga Tanzania ya viwanda".

Pia, Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya vyuo vikuu nchini(TCU) Profesa Jackobo Mtabaji, Amesema wamejipanga kuhakikisha kuwa wanafanya kazi zao kwa kusimamia mwongozo uliopo ili kuondoa mara moja huu uwepo wa vyuo vingi ambavyo havina sifa.




Harusi ya dola milioni 74, yatia hasira wananchi

Harusi moja ya kifahari nchini India ya binti ya mwansiasa mmoja imezua ghadhabu ya umma, kutokana na gharama yake wakati mamilioni ya raia wakiwa maskini.
Familia ya bwana harusi na bibi harusi wakiwa katika picha ya pamoja
Harusi hiyo iliyofanyika kwa siku tano ilifadhiliwa na mwekezaji mashuhuri ambae pia alikua Waziri katika jimbo moja India, G Janardhana Reddy.
Mwanasiasa huyo aliandaa kwa heshima ya binti yake aliyekua bibi harusi bi, Brahmani na iligharimu dola milioni 74.
Kadi za mwaliko ziliremebeswa kwa dhahabu, huku wageni wakitumbuizwa na wasanii kutoka Bollywood.
Watu wengi wamelalamikia harusi hiyo kama kejeli kwa masikini na onyesho la utajiri.Ilifanyika wakati serikali ya India ilipotangaza kuondoa sarafu ya rupee ya 500 na 1000 kama hatua ya kuchunguza mali iliyopatikana kwa njiya isiyo halali.
Mamilioni ya raia wa India wamekua wakipiga foleni kubadilisha sarafu zao na wengi wamelalamikia hatua ya serikali.Harusi nchini India huwa za kifahari na gharama zote hulipiwa kwa pesa taslimu.

Bwana Reddy ametetea heshima yake kwa bintiye akisema ilimbidi kuuza baadhi ya mali zake zilizoko, Bangalore na Singapore ili kugharamia harusi hiyo. Aidha amesema malipo yote yalifanyika miezi sita kabla ya harusi kufanywa.

Licha ya kujitetea , raia wengi wamelalamikia kwenye mitandao ya kijamii.
Baadhi ya wakosoaji wa serikali wametaka chama tawala cha Waziri Mkuu Narendra Modi cha 'Bharatiya Janata Party' {BJP}, kuwachunguza wanachama wake dhidi ya ufisadi.
Bwana Reddy aliwahi kufungwa jela miaka mitatu kwa makosa ya ufisadi. Aliachiwa huru kwa dhamana mwaka uliopita. Hekalu ambapo harusi hiyo iliandaliwa zilirembeshwa kwa dhahabu na michoro maalum iliyotungwa na waandaa filamu kutoka Bollywood.
Kuna magari maalum ya kifahari pia iliyowasafirisha wageni waalikwa.
Hapa ni baadhi ya harusi ghali zaidi duniani:
  • Vanisha Mittal, bintiye mtu wa pili kwa utajiri India Lakshmi Mittal, alimuoa Amit Bhatia katika sherehe iliyogharimu $74m mwaka 2004.
  • Harusi ya Mwanamfalme Charles na Diana wa Uingereza mwaka 1981 iligharimu £30m ($37.2m), kwa fedha za sasa ni karibu £116m. Harusi ya mwana wao William na Kate Middletoniligharimut £20m, according to the Daily Mail.
  • Harusi ghali zaidi ilifanyika Urusi mwezi Machi, kati ya mwana wa bilionea Said Gutseriev aliyemuoa Khadija Uzhakhovs mjini Moscow. Alitumia $1.2m kwa mavazi ya harusi pekee. Wageni walitumbuizwa na watu wanamuziki watatu mashuhuri: Jennifer Lopez, Sting na Enrique Iglesias. Gharama ilikuwa dola bilioni kadha.


Chanzo cha habari bbc swahili..

Hizi ndizo ndoa ghali zaidi za watu maarufu duniani

Ndoa ni kiungo pekee katika maisha ya mwandamu, na maisha yanaweza kuwa ya ajabu sana katika uso wa dunia endapo hakutakuwa na muunganiko wowote wa watu wawili wenye jinsia tofauti mbili (mwanamme na mwamke) na hawa kuridhia katika kuoana na kuishi pamoja kama mume na mke.

Duniani kumekuwa na ndoa nyingi, zikiwemo za gharama za chini, katikati na juu. 

Hebu leo tutazame ndoa za mastaa duniani ambazo zimeweza kuweka rekodi duniani kwa kuwa ghali zaidi.

Mpangilo huu upo katika orodha ya ishirini kushuka mpaka ya kwanza(top 20).
                                                                                                    

#20 Nicole Kidman & Keith Urban
Ndoa hii ilifungwa katika kanisa la katoliki (cliff-top Roman Catholic Church) uliopo katika mji wa Sydney, kwao Kidman nchini Australia, juni 25, 2006.









Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - $250,000


#19 Marc Anthony & Dayanara Torres

Baada ya kufunga ndoa ya ghafla huko Vegas, Mei 2000, Hawa wawili waliweza kufunga ndoa rasmi na kubwa katika viunga vya San Juan uiopo katika mji wa Puerto Rico hapo baadae disemba 2002.



Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - $500,000

#18 Tommy Mottola & Mariah Carey
Ndoa hii ilifungwa kati ya mwanamuziki Maria Carey na aliyekuwa mfanyakazi katika kampuni ya Sony Music, bwana Tommy Mottola mwezi juni 1993. Ndoa kufungwa katika kanisa la St. Thomas Episcopal. Ndoa hii inatafisiriwa kuwa na hadhi ya kifalme.



Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - $500,000



#17 Dario Franchiti & Ashley Judd
Hawa wawili waioana mnamo mwaka wa 2001 katika kasiri ya Skibo uliopo Skotilndi, Judd na Franchiti walihitaji kitu, mahusiano ya karibu. Cha ajabu hawa wendanao waliweza kukodi vyumba 40 katika kasiri na kugharimu dola la marekani $35,000/ kwa siku nne walizokaa hapo.


Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa :- $750,000


#16 David Beckham & Victoria Adams
Walioana Julai 1999 katika kasiri ya Luttrellstown karibu na Dublin, hii ndoa ni mwana kandanda maarufu and aliyekuwa mwanamziki wa kundi la Spice Girl na tarajio lao lilikuwa wafunge ndoa yenye hadhi ya kimalkia na kifalme. Na ndicho walichokifanya kwani sherehe yao ya ndoa ilifana sana na kuwa kama walipnda iwe.






Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - $800,000


#15 Brad Pitt & Jennifer Aniston
Ilikuwa ni ndoa ya aina yake kwa mwaka wa 2000, July 29 kati ya hawa mastaa na waigizaji wa hollywood iliyofanyika katika viwanja vya Malibu ya mwandaaji wa televisheni, Marcy Carsey. Na kila aliyehusika na kuhudhuria alitakiwa kusaini dola milioni $1 kwa ajili ya kuhifadhi unyeti wa swala. pia sherehe ilipndezeshwa busatni nzuri yenye maua mazuri bi ghali, na inasmkana idadi ya maua ilikuwa kama 50,000 na kumulikwa na mishumaa meupe yakimulika ema zuri lililokuwa katika eneo la mapokezi.

Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milioni $1


# 14 Tori Spelling & Charlie Shanian
Hii pia ni sherehe ya ndoa kati ya hawa wapendanao, Tori Spelling & Charlie Shanian iliyofanyika julai 2004. Maharusi hawa walipendeza kwa mavazi yao ya bei ghali na shela nzuri yenye bei ghali, huku mapambo mazuri ya glasi, mbao na mawe yakiwa yametawala mazingira na nakshi nzuri za maua zenye madini ya almasi zilizovaliwa kuficha uso wa maharusi.




Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milioni $1


# 13 Donald Trump & Melania Knauss
Mfanyabiashara wa mali zisizohamishika mogul na mwanamitindo walifunga pingu za maisha katika kanisa la Episcopal lilipo katika kingo za bahari huko Bethesda mnamo mwezi wa januari 2005. Mavazi ya maharusi ndiyo aliyokuwa jambo la kuongelea hapo, na kuteka mjadala. Na mavazi ya bibi harusi yaliandalia kwa namna nzuri na kugharimu pesa nyingi sana. Na baada ya sherehe, magari maarufu kwa jina la limo, wageni walisafirishwa kutoka kanisani mpaka ukumbi wa hadhi uliopo katika viunga vya Mar-a-Lago estate unaomilikwa na bwana harusi Trump, wenye thamani dola milioni $42. Huku katika sherehe hizo zikitawaliwa na wanamuziki na watumbuizaji bendi kubwa duniani.

Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : milioni $1

#12 Madonna & Guy Ritchie
Hii ndoa ilikuwa im
erembwa na maarufu kati ya wawili hawa. Walipata kuoana desemba 2000 huko Skotilandi katika kasiri ya skibo. Ndoa ilijikita katika mahusiano yasiyo ya siri, ambapo hawa wapendwa waliweza kukodi kasiri nzima, ikiwemo kukodi vyumba vyote vya wageni, pamoja na walinzi wapatao 70 na wahudumu. Bibi harusi akiwa amevalia mavazi ya ghali zaidi kwa yakiwa na nakshi ya almasi ambapo inasvmekana iliwahi kuvaliwa na malkia Grace wa Monaco. Huko bwana harusi Guy Ritchie amevalia vazi zuri ya kilti.


Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milioni $1.5



#11 Pierce Brosnan & Keely Shaye Smith
Muigizaji na mwandishi wa habari wa runinga nj
e ya miinuko ya Irelandi ogasti 2001. Huko mapokezi yakipambwa na desturi za watu wa Ireland(Irish), vyakula na michzo ikwa ya tamaduni ya watu wa jamii hiyo katika kasiri ya Ashford liloko pwani. Huko bibi na bwana arusi wakiwa katika mavazi yao ya nguvu na ghali zaidi.








Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milioni $1.5 


#10 Eddie Murphy & Nicole Mitchell
Mch
eshi na bibi harusi waliweza kuoana Hotli ya New York Plaza mnamo 1993. Zaidi ya wageni 500 waliohudhiria ukumbini hapo, ukumbi ulipambwa zulia jeupe na maua mazuri yakitanda eneo la tukio. Baada ya sherehe ya harusi pale ukumbini, wageni waalikwa waliweza kupata chakula na vinywaji vya gharam za juu.











Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milioni $1.5


#9 Tiger Woods & Elin Nordegren
Mch
ezaji wa golf  mwanamitindo wa Swedeni walioana mwaka 2004 katika bichi ya Sandy Lane Beach Resort huko Barbados. Ili kuona ndoa yao inafanikiwa kama walivyotaka hawa wawili waliwza kukodi hii shmu ya starehee na vyumba vaak vyote200 ambayo iligharimu dola $1 laki mbili. Huku mapokezi ikipambwa na mziki mzuri na mapambo ya thamani sana.










Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milioni $1.5

#8 Michael Douglas & Catherine Zeta-Jones
Ilikuwa nayo ni moja ya ndoa zilizotia fora, kwa maana vyombo vya habari vilimzunguka bwana harusi Douglas na bi haarusi Zeta-Jones mpaka sh
erehe ya harusi ilipofika ukingoni. Maharusi walichagua kufunga pingu za maisha katika hoteli maarufu kwa jina la Plaza Hotel huko New Yorks Novemba, 2005. Ili wanandoa waweze kuvinjari pasipo shida wakamua kukodi walinzi 50 wakiwemo askari polisi 30. Huku wageni waalikwa wakiwa wanawasili ukumbini kwa kadi zilizoandalia kwa nakshi nzuri za madini.





Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milioni $1.5 

#7 Elton John & David Furnish
Mwanamziki nguli wa mziki jamii ya pop na muaandaji filamu walipata kufunga ndoa d
esemba 200 wiki hiyo ya kwanza ambapo ndoa za jamii wanaounga ndoa za jinsia moja ilipopitishwa kisheria huko nchini Uingereza. Hawa wawili waliweza kubadilishana mawili matatu katika ukumbi mmoja mkubwa na mashuhuru hapo nchini Uingereza  ujulikanao kwa jina la Windsor's Guildhall, ambapo mtoto wa kiume wa kifalmPrince Charles na  Camilla Parker Bowles walipata kuoana miezi 8 iliyopita. Zaidi ya wageni 600 waliohalikwa walihudhuria wakala na kunywa chakula na vinywaji vya gharama, ambapo inakadiria kila kinywaji maarufu kama vintage pink champagne iligharimu dola $ 300 kwa kila chupa.

Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milioni $1.5 

#6 Christina Aguilera & Jordan Bratman
Baada ya Bratman kumwomba uchumba siku ya wap
endanao (Valentine's Day) huko Carmel. Wawili hawa waliweza kubadilishana maneno mawili matatu katika bonde moja maarufu kama "Napa Valley's Staglin Family Vineyard" mnamo Novemba 2005. Wawili hawa walipata kupumzika katika vibanda vya Auberge du Soleil, vinavyodaiwa kugharimu dola $3,500 kwa usiku mmoja, vikiwa na moto uliokokwa nje yao. Lakini ndoa halisi ilifanyika katika mahema yaliopo katika sehemu iliyozungukwa na barafu. Na maua ya aina mbalimbali kama rose, shaba, almasi n.k yakitawala mandhari hayo pia.

Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milioni $2

#5 Elizabeth Taylor & Larry Fortensky
Elizabeth Taylor aliw
eza kuoana mume wake wa saba ikiwa ni moja ya ndoa iliyofujisha hela nyingi sana. Wawili hawa walikutana huko kliniki ya Betty Ford Clinic, na kuoana Octoba 6, 1991 katika ranchi moja ya Michael Jackson's Neverland Ranch. Pia wawili hawa waliweza kuuza baadhi ya picha zao za sherehe maarufu kwa bei ghali zaidi ya dola milioni $1 kwa kampuni moja ya habari maarufu kwa jina la "People Magazine" ambapo hela hiyo waliigeuza kuwa mchango kwa waathirika wa Ukimwi (AIDS charities).

Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milioni $2


#4 Tom Cruise & Katie Holmes
Ndoa ya TomKat ilivuma na kuwa kama ndoa ya mwaka 2006. Wawili walipata kuoana Novemba nchini Itali katika kasiri ya 15th-century Odescalchi Castle uiopo nj
e mwa mji wa Rome. Waandishi wa habari walilijaza eneo la tukio. Wote bwana na bibi harusi wakivalia mavazi yaliosanifiwa na msanifu mavazi Giorgio Armanai kwa thamani nyingi sana. Wageni waalikwa wakiwa wakijivinjari na chocolate nyeupe, keki ya harusi na 300 chupa ya vinywaji za wine. Burudani za musiki wa okstra (orchestra ).




Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milioni $2 

#3 Elizabeth Hurley & Arun Nayar
Mwanamitindo na muigizaji wa filamu pamoja na mfanyabiashara wa kihindi walipata kuoana Machi 2007 huko sh
erehe ikiwa ikiendelea kwa siku 8 na kuvuka mabara mawili. Sherehe ya kwanza ilifanyika Machi 2 katika kasiri ya Sudeley Castle huko  mjini Gloucestershire. Baada ya sherehe yao huko Uingereza waliweza kuamia nchini India mnamo  Machi 9, ambapo sherehe za harusi zikafanyika katika tamaduni na desturi za kiindi na hii sherehhii ilifanyika Umaid Bhawan Palace katika jiji la Jodhpur, India. Ambapo hawa wawili waliweza kupumzika katika hilo jumba la kifaari kwa dola $10,000 kwa usiku mmoja.

Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milioni $2.5



#2 Paul McCartney & Heather Mills
Aliyekuwa muimbaji wa mziki wa rock katika bendi ya Beatles(Beatles band) aliomba uchumba kwa mwanamitindo Heather Mills mnamo 2001 kwa kumvisha pete ya uchumba ya almasi. Na baadae kuoana mwezi Juni 2002 kanisani St. Salvador's Church huko Monaghan, nchini Ireland. Maarusi walimachi baina ya viti hapo kanisani huku ukiimbwa wimbo wa McCartney aliomwandikia mchumba wake wenye jina la "Heather". Mapokezi yaliandaliwa na kupambwa kwa hadhi ya kihindi iliyofanyika huko kingo ya ziwa, huku watumbuizaji wa muziki wakivalia kwa tamaduni za  kihindi, na kupata milo ya watu wa jamii ya kivejitariani(vegetarian feast).

Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milioni $3

#1 Liza Minelli and David Gest
Mshindi wa tuzo za Oscar na mwigizaji, mwandaaji wa vipindi wa runinga walioana Machi 2002 kanisani Manhattan's Collegiate Church. Tukio la ndoa yao ilivuma sana, ambapo Best Man alikuwa ni Michael Jackson (ambaye ni rafiki wa karibu wa Minelli) na matroni wa bibi harusi alikuwa Elizabeth Taylor. Jackson aliambatana na Minelli wakitembea baina ya viti mle kanisani, huku wimbo wa muimbaji na mtunzi wa nyimbo Natalie Cole alipoimba wimbo wake maarufu kwa jina la "Unforgettable". Wageni waalikwa wa Minelli na Gest walikadiriwa walikadiriwa kiasi 850 ambapo waliweza kuhudumiwa vizuri. Keki ya ndoa ya ngazi 12 ikipambwa na picha ya bwana na bibi harusi. Wakati huo mziki mkubwa wa okestra(orchestra), na wasanii na waimbaji wengi kama Tony Bennett, Stevie Wonder na Natalie Cole wakitoa burudani ya kukata na shoka. Baadhi ya wafanyakazi wapatao 500 waliajiriwa kwa kuhakikisha sherehe inastawi na ulinzi umehimarika eneo la tukio. Na hii ndiyo ndoa inayokadiriwa kuwa ghali zaidi kuliko za hawa watu maaarufu(mastaa) duniani. Hata hivyo hii ndoa ya hawa wawili haikupata nafasi ya kuishi kwa mda mrefu, kwani ilivunjika mwaka uliofuatia.

Gharama za haraka za arusi inakadiriwa kuwa : - milion $3.5

Chanzo cha habari ni romancefromtheheart.com na Forbes.com