Jumapili, 6 Novemba 2016

Trump aondoshwa jukwani akiwa anahutubia

                                   
                                               
Bwana Donald Trump ambaye ni mgomba urasi nchini Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican, ameimarisha mkutano wa kampeini zake mjini Nevada hii ni mara ya walinzi wake kumuondoa jukwaani akihutubia.

Maojiano kati ya waandishi wa habari na wafuasi wake waliokuwepo katika tukio wamesema kuwa walinzi wake walifanikiwa kumuondoa jukwaani kwa hofu ya uwepo wa mtu aliyekuwa amejihami kwa silaha miongoni mwa wasikilizaji waliohudhuria katika kampeni hizo za hatua ya mwisho kabla ya uchaguzi unatarajiwa kufanyika novemba 8, mwaka huu.

Bw.Trump alikuwa anakaribia kilele cha hotuba yake ndani ya ukumbi wa Reno uliyojaa wafuasi wake, na ghafla kukatokea rabsha(purukushani) karibu na jukwaa.
Basi wafuasi wake waliyojawa na hofu na uwoga walianza kukimbilia lango la kutoka nje wa ukumbi huo kufuatia madai ambayo hayakudhibitishwa

Hata hivyo polisi wamemkamata mtu mmoja kufuatia tukio hilo lakini akaachiliwa muda mfupi baadaye.

Licha ya mtu huyo kumatwa na polisi, ila hakuweza kupatikana na silaha kama ilivyodaiwa.
Pia taarifa zinasema kuwa wagomba wot wawili (Trump na Clinton) wameimarisha kampeini zao katika jimbo muhimu la Florida. Mji wa Florida na Nevada zina umaarufu wa kuamua mshindi wa uchaguzi wa uraisi

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema huenda hatua hiyo ikamnufaisha Bi Clinton. 
Trump amesema atazuru jimbo la Minnesota ambalo chama cha Republican hakijawahi kupata ushindi kwa zaidi ya miaka arobaini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni