Jumamosi, 5 Novemba 2016

Maajabu ya mti wa Mlonge

Kwa kuanza mlonge ni nini?
Mlonge ni mti wa jenasi(nasaba) ya pekee ya moringa,
familia ya moringaceae(mimea iliyo na mnasaba ya mlonge).
Na spishi yake ni M. aleifera.
Vilevile mmea huu wa mlonge una mche ambao unatoa maajani mawili,
wenye rangi ya kijani
Mti wa mlonge katika muonekano tofauti...






Sasa tuone faida zitokazazo na mti huu wa mlonge...
Wataalamu wengi duniani wa tiba ya asili na afya kwa ujumla wameweza kubaini faida za mti huu wa mlonge kama ifuatavyo.

* Mlonge una madini ya chuma mara 25 zaidi ya spinach.
* Mlonge una potasiamu mara 15 zaidi ya ndizi.
* Mlonge una kalsiamu mara 17 zaidi ya maziwa ya ng'ombe.
* Mlonge una vitamini A mara 10 zaidi ya karoti.
* Mlonge una protini mara 4 zaidi ya mayai
* Pia mti hu wa mlonge una vitamini A, C, B, B2, B3 na E.
* Una omega 3, 6 na 9
* Mlonge unana madini muhumu za zinki , ambazo mwili katika kuongeza homoni za kiume      nguvu za kiume pia.
* Mlonge una asidi amino ambazo ni mahimu katika muungamaniko na usatawi wa mwili.

Mlonge inaweza kuimarisha mifupa kutokona na madini ya chuma iliyonayo

Mti huu una sifa moja kubwa kuwa, kuanzia mizizi yake, magome(magamba) yake, majani yake, maua yake, mbegu zake ni tiba tosha na iliyo kamili.

Kwani inakadiriwa kuwa mti wa "mlonge" unaweza kutibu magonjwa zaidi ya 300 duniani.

Haya ni baadhi ya magonjwa ambayo yanaweza kutibiwa kwa mti huu wa mlonge

# Kansa.
# Malaria.
# Athma.
# Maumivu ya mwili.
# Kisukari.
# Mwili kuwaka moto ama kupooza.
# Kifua kikuu.
# Maambukizi ya macho, ama magonjwa ya macho.
# Kisonono.
# Kuhara damu.
# Mogonjwa ya mifupa.
# Mumivu kwenye maungio.
# Manjano.
# Kipindupindu.
# Maonjwa ya ngozi.
n.k.




               Picha ya supu ya maganda ya mlonge..

Unaweza kuanda supu ya maganda yake yenye mbegu na ukatumia.

Pia utayarishaji mwingine ni kuchemsha majani yake kama mboga na ikaliwa, japo yanaweza kuwa machungu.
Pia unaweza kumenya ganda lake na kutoa punje zake 3 ukatafuna na kunywa maji. Fanya hivyo mara tatu kutwa utaona faida mapema.
Kwani mbegu zake zina kinga ya CD4 kama una tatizo hilo. Lakini hata kama hauna tatizo la kinga ya mwili, unaweza kuimarisha kinga ya mwili wako kwa kufanya hivyo. 





                                             Unga wa majani ya mti wa mlonge

Vilevile unaweza kuandaa unga unaotokana na majani ya mlonge kwa kuhakikisha umeanika kivulini na sio juani ili unga uwe wa kijani zaidi kwa ubora wake. 
Tia unga wako ulosaga katika vimiminika kama uji, chai, maji ya kunywa hasa ya uvuguvugu, na hata kwenye chakula kama wali, ndizi, ugali n.k.
Unaweza kuanza na kujiko kimoja na kuendelea kulingana na wingi wa chakula ama idadi ya watumiaji.

Asante kwa kufuatilia machapisho ya Zjuie izi. www.zijueizi.blogspot.com
Karibu tena na waweza kuchangia kwa kukoment hapa chini.

Maoni 4 :

  1. Maoni haya yameondolewa na mwandishi.

    JibuFuta
  2. Thanks for sharing with us, and lovely explanation.

    JibuFuta
  3. Napenda kujua kama unaweza kusaga majani ya mlonge ukanywa kama juice

    JibuFuta
  4. Vipi kuhusu fangasi sehemu ya sili inatibu na kama inatibu matumizi yake yanakuaje?

    JibuFuta