Jumatano, 9 Novemba 2016

Hatimaye mh. Donald Trump kupokea kijiti toka kwa raisi Barack Obama


Baada wananchi wa Marekani kupiga kura.
Trump ameibuka mshindi baada  kupata kura nyingi kutoka majimboni baada ya kupata kura 279 mpaka sasa na Hillary Clinton kuwa na kura 218 ya matokeo ya majimbo 46 kati ya 50

Bi Hillary Clinton akubaliana na matokeo hayo.

Ni uchaguzi uliokuwa na mchuano mkali sana kati ya vyama hivi viwili vilivyokuwa na wafuasi wengi na kuvuta hisia kali ndani na nje ya nchi ya Marekani.. Na hii tuliweza kushuhudia kipindi cha kampeni.

Chama cha Republican kilichowakilishwa vyema na bwana Trump, huku bi Hillary akiwakilisha Democrats nayo kwa umakini wake.

Matokeo mengine ni kama ifuatavyo...

Kwa Republican wameweza kujizolea maseneta 51, huku chama cha Republican kikijinyakulia 47, Kwa upande wa matokeo ya kura za wakilishi ambao nao ni muhimu katika serikali ya shirikisho, chama cha Republican kimejizolea wawakilishi kura za 236, huku washindani wao wa karibu Democrats kujitwalia 191 ambapo kwa sera na sheria zao unatakiwa kuwa kura za wawakilishi 218.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni