Jumatano, 23 Novemba 2016

Samata na Wanyama nje Tuzo za CAF.

Shirikisho la soka barani Afrika CAF limeachia orodha ya wasaka kandanda watano ambao wataweza kushindania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2016.
Orodha hii imeamuliwa na kura za wajumbe wa kamati ya vyombo vya habari vinavyotambuliwa na CAF, na kamati ya maendeleo ya ufundi ya CAF, pamoja na jopo la wataalamu ambao huwa ni nusu ya 20(watu 10). Tuzo hizo zitafanyika January 5 2017, mjini Abuja Nigeria.
Wafuatao ni orodha ya wachezaji watakaoshindania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika wa Mwaka,
  •        Pierre-Emerick Aubameyang  (Gabon na Borrusia Dortmund)

  •       Riyad Mahrez (Algeria na Leices)

  •      ➤ Sadio Mane (Senegal na Liverpool)

  •       Mohamed Salah (Egypt na Roma)

  •       Islam Slimani (Algeria na Leicester).

Mbwana Ally Samatta, ni mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayechezea soka ya kulipwa Ubelgiji ni miongoni mwa wachezaji aliyekuwa kwenye orodha ya wachezaji 30 ambao walipata kuteuliwa kushindania tuzo ya shirikisho la soka barani Afrika (CAF) ya Mchezaji Bora wa Afrika katika awamu ya kwanza kabla ya wachezaji hao kupunguzwa hadi watano.
Victor Wanyama, ambaye ni kapteni wa timu ya taifa la Kenya, na kwa sasa anachezea klabu ya Tottenham. Mchezaji huyu naye alikuwa kwenye orodha iliyoteuliwa na CAF kabla ya mchujo huo haujatokea.
Wafuatao ni orodha ya wachezaji watakaoshindania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika wa Mwaka anayecheza ligi za ndani ya Afrika,
    Khama Billiat (Mamelodi Sundowns na Zimbabwe)
    Keegan Dolly (Mamelodi Sundowns na South Africa)
    Rainford Kalaba (TP Mazembe na Zambia)
    Hlompho Kekana (Mamelodi Sundowns na South Africa)
    Denis Onyango (Mamelodi Sundowns na Uganda).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni